Shilole Awapa makavu Wanaume "Si Kila Mwanamke ni Chombo cha Starehe"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shilole Awapamakavu Wanaume "Si Kila Mwanamke ni Chombo cha Starehe"
Msanii wa BongoFleva na mjasiriamali nchini Tanzania, Zuwena Mohamedy maarufu kama 'Shishi Babe', amewaonya wanaume wote kuacha tabia ya kuwaona wanawake kama chombo cha starehe, na badala yake amewataka waishi kiakili na wanawake zao kusudi waweze kuwavushana kwenye mafanikio yao.

Shilole ametoa onyo hilo kupitia ukurasa wake wa kijamii mchana wa leo Agosti 31, 2018, baada ya kuwepo wimbi kubwa la wanaume hususani waliopo kwenye ndoa au mahusiano ya kimapenzi, kutowaheshimu wanawake kutokana na maumbile yao huku wengine wakijisahau kuwa hakuna mafanikio yoyote bila ya uwepo wa wanawake hao.

"Sio kila mwanamke unayemuona ni chombo cha starehe, wengine ni ufunguo wa mafanikio yako. Heshima kwa wanaume wote wanaoheshimu wanawake", ameandika Shilole.

Katika baadhi ya jamii kumekuwepo na vijitabia vidogo vidogo ambavyo humchukulia mtoto wa kike kutokuwa na thamani, kwa kile wanachokiamini kuwa wanawake wameumbwa kwa lengo la kuwapa starehe tu hapa duniani nasio kuwapa changamoto katika kujiendelea kiuchumi uchumi wa maisha na kutaka kula starehe peke yake bila ya kujali kesho yao.

TAZAMA VIDEO MPYA YA ROSA REE HAPA CHINI ALIYOTOA LEO..
HAYO MAUNO SI YA NCHI HII:




-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad