"Siwezi Kupotezwa Situmiki Kisiasa"Nikki wa Pili Afunguka Makubwa

Siwezi Kupotezwa- Nikki wa Pili
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amedai sio rahisi kwa yeye kuweza kupotezwa kwenye 'game' ya muziki, kutokana na kuweka hadharani nia yake ya kujiingiza katika masuala ya kiungozi kama baadhi ya watu wanavyomfikiria.

Nikki ametoa kauli hiyo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv baada ya kuzuka mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii juu ya suala hilo, huku wengine wakidai huenda msanii huyo anatumiwa kisiasa jambo ambalo litaweza kuja kumpoteza katika muziki bila ya yeye kujijua.

"Mtu akiwaza kuwa natumika kisiasa nafikiri hilo litakuwa ni tatizo lake la kufikiria, mimi sioni kama kuwa na ndoto ni kutumika na mtu yoyote. Kuwa na ndoto ni asili ya binadamu na kila mtu ana mapokeo yake pamoja na muelekeo. Sidhani kama jambo hili linaweza kuniathiri kwa chochote kile katika kazi zangu za kisanaa au kunipoteza katika soko", amesema Nikki wa Pili.

Aidha, Nikki wa Pili amesema kuwa licha ya kufahamiana na watu wengi mbalimbali, lakini hakuna yeyote aliyeweza kujitokeza kumshawishi juu ya mambo ya kujiunga na chama fulani ili aweze kupigania malengo yake ya kuwa rais kwenye miaka ya huko mbeleni.

Nikki wa Pili ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wasomi nchini Tanzania na kutegemewa kwa kiasi kikubwa na mwanamuziki wenzake, katika kuwakilisha maoni yao pindi yanapotokea matukio ya kitaifa ambayo yanajumuisha wasanii wote bila ya kubagua kitu wakifanyacho.

TAZAMA VIDEO MPYA YA ROSA REE HAPA CHINI ALIYOTOA LEO..
HAYO MAUNO SI YA NCHI HII:💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad