Young Dee "Amber Lulu Hawezi Kufanya Mziki Mzuri Bila Kunitaja Mimi, Mimi ndio Daraja la kiki"

Msanii wa Bongo fleva na hitmaker wa Bongo Bahati Mbaya Young Dee ameingia Kwenye bifu zito na aliyekuwa mpenzi wake na msanii mwenzake Lulu Eugenn maarufu kama Amber Lulu.

Bifu la Amber Lulu na Young Dee lilianza Siku za nyuma baada ya Amber kumtuhumu Young Dee kwa kumpa kipigo studio baada ya kumuona akiwa na mwanaume mwingine.

Amber Lulu alimtolea povu zito Young Dee baada ya picha zake za Harusi kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Amber rapa huyo hawezi kuoa kwa sababu hicho si kitendo rahisi na ukiangalia yeye mwenyewe sasa hivi anatamani kuolewa, hivyo kumtaka afanye muziki bila kutengeneza kiki kama anaweza.

Global Publishers lilimtafuta Young Dee Baada ya povu Amber ambapo Meneja alifunguka:

Young Dee hawezi akabishana na mtoto wa kike halafu hata hivyo huyo Amber Lulu hawezi akafanya muziki mzuri bila kufanya kiki na tena ukiangalia kiki zake nyingi ni lazima amtaje Young Dee, kwa sababu anajua kuwa brand kubwa hivyo anaona akimtumia lazima atoboe”.

Amber Lulu naye alifunguka tena kuhusu Young Dee ambapo aliendelea kumtolea shombo baada ya kusema anahitaji kuolewa kwani hawezi kuoa:

Niliongea vile kwa sababu najua Young Dee hawezi akatoa wimbo bila kufanya kiki, anadanganya watu kuoa wakati yeye mwenyewe anahitaji mtu wa kumuoa, halafu ukiangalia kiki ni kubwa kuliko wimbo anaotaka kuutoa yani kiufupi siku hizi muziki wake ushakufa labda ajipange upya“.

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad