9/14/2018

Baada Ya Kumwagana Na Petit Esma Ataja Sifa Za Mwanaume Anayetaka Kuwa Naye

 Baada Ya Kumwagana Na Petit Esma Ataja Sifa Za Mwanaume Anayetaka Kuwa Naye
Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’amefunguka na kutaja sifa za mwanaume anayetaka kuwa naye sasa baada ya kumwagana na mume wake Petit Man.

Siku ya jana Esma aliweka wazi kuwa yeye na Petit waliachana kipindi kirefu kidogo na kisa cha kuachana kikiwa ni Mumewe kuzidisha kuwa na michepuko.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Esma ameweka wazi kuwa yeye ndio alimuacha Petit na kabla hajamuacha alimfuata mama yake na kumwambia matatizo ya Mumewe na kukiri kuwa mama yake alimsema sana.

Lakini pia amesema hivi sasa anatafuta nyumba ya peke yake ili aweze kuanza maisha mapya peke yake na pia ametajwa sifa za mwanaume ambaye atapenda kuwa naye Kwenye Mahusiano kwa sasa:

Kwanza  mwanaume ambaye namuhitaji ni mwanaume gentleman anayejielewa, mwenye kazi yake nzuri, Awe sio mtu wa drama na Instagram yaani Awe yule mwanaume ambaye yuko straight tunapanga kufanya kitu fulani tunafanya yaani in short nataka mwanaume anayejielewaa kama mimi mwenyewe”.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger