9/14/2018

Donge Nono Kutolewa na Takukuru kwa Atakayesaidia Kupatikana Hans Pope

Donge Nono Kutolewa na Takukuru kwa Atakayesaidia Kupatikana Hans Pope
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) imewataka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope na Frankline Lauwo kujisalimisha katika ofisi zake au kituo cha polisi kujibu tuhuma zinazowakabili.Aidha, TAKUKURU imetangaza zawadi nono kwa mwananchi atakayefanikisha kupatikana kwa Hans Pope na  Lauwo baada ya TAKUKURU kuwatafuta kwa njia za kawaida bila mafanikio.Katika kesi hiyo, ambayo inayowahusisha pia kina aliyekuwa Rais wa Simba, Evance Aveva na katibu wake, Geofrey Nyange “Kaburu”, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa TRA juu ya ununuzi wa nyasi bandia za Uwanja wa Simba SC.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger