Jina la Mapacha Watatu Lazua Ugomvi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jina la Mapacha Watatu Lazua Ugomvi
Taarifa ambazo zimetufikia ni kwamba, Khalid Chokoraa ameamua kurudisha bendi ambayo inatumia jina la Mapacha watatu licha ya kwamba jina hilo linatumiwa pia na Jose Mara kwenye bendi yake.


Kupitia eNewz, Khalid Chokoraa amesema kwamba kwa yeye ana bendi yake inaitwa 'Mapacha watatu original', ambayo wasanii walioko ndani yake ni Catty, Fagasoni pamoja na wengine wakubwa ambao wamejikusanya ili kujitafutia riziki katika kazi yao ya muziki.

Hata hivyo Chokoraa ameendelea kusisitiza kwamba "wazo la kuanzisha kundi la mapacha watatu lilikuwa langu kwa kuwa hata mwanzo mimi ndio niliwashauri kina Jose, mara kwamba tuanzishe kundi ambalo tutakuwa sisi watatu kwa pamoja na tutaliita jina la mapacha watatu hivyo naamini mwenye wazo ndio mmiliki halali".

Aidha, Chokoraa alidai walishawahi kwenda hadi BASATA kufuatilia suala hilo la umiliki wa jina ambapo wote waliruhusiwa kutumia kwa namna wanavyotaka, kwani waliambiwa kila aliyekuwa mapacha watatu ana haki na jina hilo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad