9/17/2018

Lowasa Afunguka Kuhusu Kustaafu Siasa

Lowasa Afunguka Kuhusu Kustaafu Siasa
Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowassa amekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni zikidai kuwa ametangaza kustaafu siasa kutokana na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupoteza jimbo la Monduli ambalo amewahi kuliongoza.

Akizungumza na www.eatv.tv Lowassa amesema,  hana taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Monduli kwa kuwa yuko safarini akitokea Arusha kuelekea Dar es salaam wala hajazungumza chochote kuhusiana na kustaafu siasa.

“Nani kasema maneno hayo? Mimi niko safarini sijapata 'document' yoyote kuhusu matokeo ya uchaguzi wala sijaongea popote”, amesema Lowassa.

Mapema leo yaliibuka majadiliano kwenye mitandao ya kijamii yakihusisha baadhi ya viongozi pia akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akidai kuwa amepata taarifa kuwa Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CHADEMA amestaafu siasa.

“Eti nimesikia kuwa Mzee wetu ameamua kuachana kabisa na siasa. Mh Gambo naomba uhakika wa hizi taarifa kwa sababu wewe upo karibu na Monduli”, ameandika Makonda.

Uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Ukonga na Monduli umefanyika jana Septemba 16, ambapo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Monduli kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Julius Kalanga amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo hilo kwa kupata ushindi wa kura 65,714 huku mpinzani wake Yonas Laizer wa (CHADEMA)akipata kura 3,187
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

  1. haya mashaurianoyanandelea kwa Pole pole.
    msiwe na haraka ya kudandia basi, yalitokea Hai inaosha mie huwa nnapataga mgao na bb ziro ppia.
    mie nta tangaza mwenyewe wakati muafaka.msinikatishie ulaji gafla.
    pii po pipo....

    ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger