Makene Aendelea Kusota Rumande

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makene aendelea kusota rumande
Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandao.

Akizungumza na MCL Digital wakili wa Makene, Fred Khiwelo amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana blog iitwayo Chadema.blogspot.com pamoja na maudhui yake.

“Ni kweli nimemfuatilia mteja wangu kujua haki ya kupata dhamana baada ya kushikiliwa toka jana lakini polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi na hivyo hawawezi kutoa dhamana kwa muda huu,” amesema Khiwelo.

Amesema swala la kumiliki mtandao mwanachama yeyote anaweza kuwa anamiliki kwa jina hilo, kumshikilia mteja wake kwa muda wote bila kumpa dhamana ni ukiukwaji wa sheria.

Mchana wa leo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema akizungumza makao makuu ya Chadema amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia Makene.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad