Manara Ashikwa na Tumbo, Hali si Shwari Aelekea Hospitalini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Na George Mganga

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameshikwa na homa ya tumbo ambalo limempa wakati mgumu kwa siku mbili sasa.

Manara ambaye alikuwa Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Simba dhidi ya Mbao, ameeleza kuwa tayari ameshaelekea hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

Licha ya kutumia dawa kwa ajili ya kukata maumivu, Manara amesema kuwa dawa hizo hazijasaidia chochote kile na imembidi aelekee hospitalini kwa ajili ya vipimo.

"Dua zenu aumwa sana, ninapelekwa hospitali maana hali si shwari, tumbo linasokota kwa siku mbili sasa na dawa zimeshindwa kufanya kazi" amesema Manara.

Wakati Manara akisumbuliwa na tumbo, timu ya Simba ipo mjini Shinyanga hii leo kucheza na Mwadui FC ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara majira ya saa 10 kamili jioni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad