google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mashuhuda Waeleza Jinsi Kivuko cha MV Nyerere kilivyozama | UDAKU SPECIAL

Mashuhuda Waeleza Jinsi Kivuko cha MV Nyerere kilivyozama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KIVUKO cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilaya ya  Ukerewe mkoani Mwanza kimezama ziwa Victoria.

Inadaiwa kwamba kivuko hicho kimezama kikiwa na abiria ambapo hata hivyo bado haijafahamika idadi ya abiria waliokuwemo ingawa taarifa za awali zinadai kilikuwa na abiria zaidi ya 90.

Kwa mujibu wa baadhi ya waliozungumzia kivuko hicho wamedai kilikuwa kinatokea Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.

Kwa mujibu wa mashuhuda wamedai kuwa ghafla kilianza kutitia kwenye maji kwa nyuma kulikokuwa na mzigo na kuwezesha abiria waliokuwa mbele kurukia majini na kuogelea na mitumbwi iliyokuwa pale kufanya kazi ya kuwaokoa abiria waliorukia majini.

Pia inadaiwa abiria wengi waliokuwa ndani ya Mv Nyerere hawakuweza kutoka na kuwa wamezama.

Mmoja ya waliozungumzia kuzama kwa kivuko hicho amedai idadi ya abiria waliopanda haijulikani ingawa uwezo wa kivuko ni kubeba abiria 150.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa kwani simu yake haikuwa hewani.

Hivyo tutaendelea kuwajuza kinachoendelea na idadi kamili au abiria waliokuwamo kwenye kivuko hicho.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad