Mtanzania Aliyemtandika Bondia Kutoka Uingereza Atua Kwa Staili Hii Bungeni Ajizolea Mamilion

BONDIA Hassan Mwakinyo amepewa zawadi ya Tsh. Milioni 7.72 baada ya kuchangiwa Sh. 20,000 na kila mbunge alipotembelea Bunge jijini Dodoma leo kufuatia ushindi aliyoupata hivi karibuni baada ya kumtwanga Bondia wa Uingereza, Sam Eggington kwa TKO .


Hayo yamejiri baada ya Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hilaly kuomba mwongozo wa kwa Kiti cha Spika na kusema; “Tumekuwa tukiwachangia sana mamisi humu ndani, leo hii tunaomba mwongozo wako angalau tumchangie Tsh. 20,000 kila mmoja, naomba mwngozo wako spika,” alisema Aeshi.


Wabunge waliitika kwa makofi mengi kisha Spika Job Ndugai alipitisha mwongozo huo mara moja kila mbunge atakatwa posho yake.
Mwakinyo alimtwanga Eggington ambaye aliwahi kuwa Bondia Namba moja wa Uingereza sekunde ya 45 ya mzunguko wa pili wa mchezo huo na kutangazwa Bingwa.


HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Mtanzania Aliyemtandika Bondia Kutoka Uingereza Atua Kwa Staili Hii Bungeni Ajizolea Mamilion Mtanzania Aliyemtandika Bondia Kutoka Uingereza Atua Kwa Staili Hii  Bungeni  Ajizolea Mamilion Reviewed by Udaku Special on September 14, 2018 Rating: 5

1 comment:

Powered by Blogger.