Rihanna Apata Shavu Barbados Ateuliwa Kuwa Balozi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rihanna Apata Shavu  Barbados Ateuliwa Kuwa Balozi
Good news ikufikie kutoka kwa muimbaji Rihanna ambaye ameteuliwa na serikali ya Barbados kuwa Balozi wa nchi hiyo kwenye mambo ya Kidiplomasia(Ambassador Extraordinary and Plenipontentiary), Barbados  ndio chimbuko la Rihanna.

Majukumu atakayokuwa akiyafanya Rihanna kama Balozi  ni pamoja na kutangaza mambo ya utalii, kusaidia masuala ya elimu na uwekezaji wa nchi hiyo ya Barbados ikiwa uteuzi huo ulitangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo  Mia Amor Mottley siku ya September 20,2018.

Waziri Mkuu wa Barbados alisema “Rihanna ana mapenzi ya dhati na nchi  ya Barbados na amejilenga zaidi kwenye uhisani hususani katika sehemu ya afya na elimu na pia ameonyesha uzalendo kwa kujitoa zaidi na kuthamini kisiwa hiki kama nyumbani”

Rihanna ambaye jina lake halisi ni “Robyn Rihanna Fenty” alipata mafanikio makubwa kwenye kiwanda cha urembo baada ya kuzindua bidhaa zake za “Fenty Beauty” mwaka 2017-2018 na huku mafanikio mengine aliyapata kwenye muziki.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad