Alliance FC wakiri kupewa akili na Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Alliance FC wakiri kupewa akili na Yanga
Klabu ya soka ya Alliance FC ya Mwanza inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara, imesema ubora na matokeo mazuri ya Yanga kwenye ligi, umewasaidia kupata akili za kujipanga vizuri kwaajili ya mchezo wa ligi kuu leo jioni.

Akiongea kuelekea mchezo huo utakaopigwa saa 10:00, kocha wa Alliance amesema Yanga ni timu kubwa hivyo wanaheshimu ubora wake wakiwa mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

"Tunaiheshimu Yanga kwenye ligi yetu bado haijapoteza mchezo hadi sasa na inaenda vizuri kwa hiyo inatupa akili ya kuingia kwa tahadhari ili tuweze kujihami na tusitengeneze makosa'', amesema Makata.

Aidha Makata amesema mbali na kujihadhari watatumia mbinu za kushambulia kwa kushtukiza pamoja na kutumia nafasi zote watakazozipata ili waweze kupata matokeo mazuri yatakayowakwamua kutoka nafasi ya 19 wakiwa na alama 6 pekee kwenye mechi 9.

Ameongeza kuwa wao wanajivunia kuwa timu ya kwanza yenye wachezaji wa Academy kupanda ligi kuu huku wakiendelea kutumia vijana wao na kadri siku zinavyokwenda wanazidi kupata uzoefu na watafanya vizur
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad