Kauli ya Makonda Baada ya Dar es Salaam Kuongoza Matokeo ya Darasa la Saba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kauli ya Makonda Baada ya Dar es Salaam Kuongoza Matokeo ya Darasa la Saba
Kufuatia Mkoa wa Dar Es Salaam kuongoza katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa Shule za Msingi, RC Paul Makonda ametoa pongezi kwa Walimu, Waratibu Kata, Maafisa Elimu ,Wazazi pamoja na wanafunzi.

Makonda ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuahidi kutoa zawadi kama motisha kwa Walimu.

“Nawapongeza sana sana Walimu, waratibu kata, maafisa Elimu , wazazi pamoja na wanafuzi Kwa kuunganisha nguvu na hatimae tumeongoza ktk matokeo ya darasa la saba Tanzania.Asanteni sana kwakunivisha nguo na kumpa heshima Rais wetu Mpendwa. Ofisi yangu itaandaa utaratibu wa kutowa zawadi kama motisha na Asante Kwa kazi wanayoifanya walimu pamoja na wanafunzi. Tumeongoza tena kwa mara nyingine tena,“ameandika Makonda.

Dar Es Salaam imeongoza kitaifa katika matokeo hayo kwa mwaka wa pili mfululizo ikifuatiwa na Geita, Arusha na Kilimanjaro .

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad