Kifo cha Muigizaji Mashaka, Ray na Steve watoa ya moyoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa filamu nchini Vincent Kigosi (Ray Kigosi) amesema kabla mauti hayajamkuta muigizaji mkongwe Ramadhani Ditopile maarufu kama Mashaka amesema alikutana nae maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga kumshirikisha kwenye moja ya kazi zake za filamu. 

Vincent Kigosi amesema ameguswa na msiba huo kutokana historia yake na muigizaji huyo katika kikundi cha Kaole  Sanaa Group kupitia maigizo yaliyokuwa yakirushwa kituo cha ITV. 

Ray Kigosi amesema  "Mashaka ni msanii mkubwa  na msiba wake ni mkubwa sana kazi ya mungu haina makosa, ameacha pigo kwenye tasnia ya  filamu na maigizo, maana ni mara chache sana kuwa na waigizaji kama wale." 

"Wiki tatu zilizopita nilikutana nae kariakoo na nilimwambia kuna project kubwa inakuja nataka kukushirikisha, yaani kikubwa alikuwa mtu mpole sana na mcheshi", amesema Ray Kigosi. 

Kwa upande wake Steve Nyerere akizungumza na www.eatv.tv amesema "cha muhimu nilichotaarifiwa watazika kesho, hakuna mtu ambaye hataweza kushiriki maana ni msiba wa msanii mkubwa kwa hiyo wasanii wote tutajitokeza kwa wingi kumzika ndugu yetu Mashaka". 

Mapema leo hii kulisambaa taarifa juu ya kifo cha msanii huyo wa zamani wa maigizo ambaye anafahamika kama Ramadhani Mrisho Ditopile (Mashaka), ambapo alifariki dunia katika hospitali ya amana jijini Dar es salaam.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad