10/11/2018

Messi Kuja na Tukio la Kihistoria Maishani Mwake

Messi Kuja na Tukio la Kihistoria Maishani Mwake
Nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ametangaza kuja na tamasha kubwa la kihistioria litakaloelezea maisha yake ya soka.


Tukio hilo linalojulikana kwa jina la 'Cirque du Soleil' linaloandaliwa na kampuni ya matamasha ya muziki ya Montreal litakuwa ni la kwanza kufanyika kwa upande wa wanasoka na litafanyika kuanzia mwaka 2019 ambapo litazunguka dunia nzima.

Tarehe rasmi na wapi ambapo litaanzia kufanyika, bado haijajulikana. Akizungumzia ujio wa tamasha hilo, Lionel Messi mwenyewe amesema,

"Cirque du Soleil ni moja ya familia yetu ", amesema Messi .

''Najihisi kuwa na wakati mzuri kwamba Cirque du Soleil wataandaa tamasha linalohusu maisha yangu binafsi na maisha yangu ya soka. Nina uhakika tamasha hili litawashangaza wengi kama ambavyo matamasha yao mengi yanavyokuwa.

Mchezaji huyo ameitumikia Barcelona katika maisha yake yote ya soka mpaka sasa, akiwa na mafanikio kadhaa yakiwemo kushinda tuzo ya Ballon d'Or mara nne, kombe la ligi kuu nchini Hispania 'La Liga' mara tisa na ligi ya mabingwa barani Ulaya mara nne.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger