Mkuu wa mkoa asema yeye ni zaidi ya Gattuso

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa mkoa asema yeye ni zaidi ya Gattuso
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, amesema yeye anajua sana michezo kuliko watu wanavyodhani kwani enzi zake alicheza sana mpira na alikuwa hatari kama mwanasoka mkongwe Gennaro Gattuso.


Akiongea hivi karibuni kwenye moja ya mikutano yake ya ziara mkoani Tabora, Mkuu huyo wa mkoa aliahidi kuwa ataboresha michezo mkoani humo kwani yeye ni mtaalam wa soka kama wanasoka wakongwe.

''Unajua watu wanadhani mimi sijui michezo lakini mimi nilikuwa napiga chenga mpaka naukalia mpira na nilikuwa nafunga kama Gatusso tena kwa mguu wa kushoto na nikikaa golini nakuwa kama Emmanuel Okala au Mambosasa'', alisema Mwanri.

Emmanuel Okala ni mlinda mlango wa zamani wa Enugu Rangers na timu ya Taifa ya Nigeria ambaye alicheza kwa kiwango kikubwa miaka ya 1972 na 1980.

Mkuu huyo wa mkoa amewataja wachezaji wengine ambao anafafana nao viwango kuwa ni golikipa wa zamani wa Tanzania Athuman Mambosasa pamoja na Gennaro Gattuso beki wa zamani wa AC Milan na Italia ambaye kwasasa ni kocha wa AC Milan.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad