Mwili wa Isack Gamba Kuwasili Nchini Jumatatu ya Wiki Ijayo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwili wa Isack Gamba Kuwasili Nchini Jumatatu ya Wiki Ijayo
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa zamani wa IPP media, kupitia Radio One na ITV kabla ya kuhamia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani, Deutche Well DW, Isack Gamba anatarajiwa kuzikwa Bunda mkoani Mara mapema wiki ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo  ya habari jijini Dar es salaam, mwili wa Isack Gamba utawasili nchini jumatatu ya wiki ijayo na shughuli ya kuaga mwili huo zitaanza wiki hiyo.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa upande wa Dar es salaam, msiba upo kwa dada yake, Gongo la Mboto, kituo kipya. Na kwa anayetaka kufika anaweza kuuliza Mongolandege kwa Mandai, Mbuyuni.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo mara baada ya zoezi la kuuaga mwili wa Isack Gamba mwili huo utasafirishwa kuelekea Bunda Mkoani Mara mahali alipozaliwa kwa ajili ya mazishi ya mwili wake.

Oktoba 18 mwaka huu kulisambaa taarifa juu ya kifo cha mtangazaji nguli wa zamani alikutwa akiwa amefariki nyumbani kwake mjini Bonn Ujerumani ambapo ilisadikika kabla ya kubainika kwa kifo chake mtangazaji huyo hakufika ofisini kwa takribani siku tatu.

Kwa mujibu wa mfanyakazi huyo alisema Isaac Gamba hakuonekana kazini asubuhi, ndipo watu wa ofisini wakaenda kutoa taarifa polisi, waliofika nyumbani kwake na kuvunja mlango wakamkuta Gamba amefariki tayari.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad