google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html NECTA Yatangaza Matokeo ya Darasa la 7.....Yatazame Hapa | UDAKU SPECIAL

NECTA Yatangaza Matokeo ya Darasa la 7.....Yatazame Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi na kubainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 4.96.

Ufaulu mwaka 2017  ulikuwa asilimia 72.76 na 2018 ni asilimia 77.72.

Akizungumza leo Jumanne Oktoba 23, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 733,103 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

“Watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 waliotunukiwa matokeo wamefaulu. Watahiniwa hawa wamepata alama 100 au zaidi kati ya alama 250," amesema.

Amesema kati ya hao wasichana ni 383,830 (asilimia 77.12) na wavulana ni 350,273 (asilimia 78.38).

"Takwimu zinaonyesha kuwa ufaulu katika masomo ya Kiingereza, Maarifa ya jamii, Hisabati na Sayansi umepanda kwa asilimia kati ya 4.03 na 11.92 ikilinganishwa na mwaka jana," amesema.

Ameongeza kuwa ufaulu katika somo la Kiswahili umeshuka kwa asilimia 1.44.

Pia, Necta imewafutia matokeo watahiniwa 357 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani yao na 120 hawakufanya kabisa na watarudia mwakani.

==>>Kutazama matokeo hayo

Bofya hapa === > Matokeo Darasa la Saba 2018 (Link 1)

Bofya hapa === > Matokeo Darasa la Saba 2018 (Link 2)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad