10/12/2018

Watu 12 Wamekamatwa Kutekwa kwa Mo DewijKamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu wanaoshikiliwa kwaajili ya mahojiano kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji 'MO Dewji' wamefikia 12.

Akizungumza na www.eatv.tv, Mambosasa amesema kuwa hadi sasa watu 12 wameshikiliwa ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo lililotokea mapema leo alfajiri, kati ya hao waliokamatwa ni pamoja na walinzi wa hoteli ya Collesium, mahali ambapo tukio hilo limetokea.

"Kwa sasa wako 12 wakiwamo walinzi wote watano wa Kampuni ya G1 inayosimamia ulinzi wa hoteli hiyo, pia kuna security Manager (afisa usalama) wa hoteli," amesema Mambosasa


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger