11/30/2018

Akiwa na Umri wa Miaka 19 tu, Mrembo Lynn Atamani Kuolewa

MUUZA nyago maarufu Bongo aliyetimiza miaka 19 hivi karibuni, Irene Godfrey maarufu kama Lyyn ameweka wazi kuwa anatamani kuolewa hata sasa.

 Akizungumza na Ijumaa, Lyyn aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alisema kwamba japokuwa ndoa ni mipango ya Mungu lakini yeye anatamani sana kuolewa na kutulia katika ndoa yake kwa sababu itamuepusha na mengi ambayo anazushiwa sasa.


“Unajua zamani malengo yangu yalikuwa kuolewa nikiwa na umri wa miaka 26 lakini kila siku zinavyozidi kwenda ndio nazidi kutamani ndoa kwa kweli sijui kwa sababu mtu wangu ananijali sana na kunipa mapenzi ya kweli, ingawa sitakuja kuweka mahusiano yangu wazi kwa sababu bebi wangu hapendi labda mtakuja kumjua tukioana,”alimaliza kusema Lyyn.Lyyn aliwahi kuliambia Ijumaa kuwa anajivunia kutimiza miaka 19 akiwa na magari kadhaa ya kifahari pamoja na ghorofa moja.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger