google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Asilimia 96 ya Walioajiriwa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ni Watanzania | UDAKU SPECIAL

Asilimia 96 ya Walioajiriwa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ni Watanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Asilimia 96 ya Walioajiriwa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ni Watanzania
Zaidi ya watu 6,000 wameajiriwa katika mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR). Kati ya ajira hizo asilimia 96 sawa na watu 6,182 ni za Watanzania na asilimia nne sawa na watu 258 ni wageni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 14, kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kwa upande wa wataalamu 189 ni Watanzania na 258 ni wageni.

“Ajira 626 za Watanzania wasio na ujuzi na 19 za wenye ujuzi zimepatikana kupitia kampuni za wazawa wanaoshiriki moja kwa moja kwenye mradi huu, hivyo tunafanya vizuri sana,” amesema Kadogosa.

Amesema maendeleo ya ujenzi huo kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro yamefikia asilimia 34.

Kipande hicho chenye urefu wa kilomita 300 kilianza kujengwa Mei 2, mwaka jana na kinatarajiwa kukamilika Novemba 2, mwakani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad