11/09/2018

Baada ya Zari Kupata Dili Nono Uganda..Aamua Kutoa Shavu Hili

HUENDA jina la Zari likawa linamaanisha zali kwani si kwa kupata mazali ya mentali kiasi hiki! Siku chache baada ya kuwa MC katika Tuzo za African Leaders 4 Change huko Afrika Kusini akiwa pembeni mwa baba wa staa wa R&B, Beyonce Knowles, Mathew Knowles, mwanamama mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ametoa shavu kwa mashabiki wake nchini Uganda.

Zari ameyafanya hayo muda mfupi baada ya kupata zali la kuwepo katika vivutio vikubwa vya utalii nchini humo akiwa kama balozi wa utalii ambapo atatembelea katika mbuga kubwa za wanyama pamoja na chanzo cha Mto Nile pande za Jinja.

Akizungumzia ishu hiyo ndani ya Hoteli ya Serena nchini Uganda, Zari alisema ili kuwavutia watalii na watu wengine ameona kuwa na kampeni maalum ya kuwashirikisha mashabiki wake na kampeni hiyo ameiita jina la Tulambule Ne Zari akimaanisha Tutembee Na Zari.

“Niambie sehemu unayopenda kutembelea Uganda, unaweza ‘ku-google’ vivutio vyote vya utalii Uganda na ukasema ni sehemu gani unapenda kutembelea,” alisema Zari na kuongeza: “Nitatoa ofa ya gharama zote za safari na ujue tu mimi ni Boss Lady kwako na kwa mwenzako au familia yako.”

GPL
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger