HAYA Hapa Maajabu Saba ya Mbegu za Maboga Ambayo Watu Wengi Hawayajui..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbegu za maboga hutokana na tunda liitwalo boga, tunda ambalo asili yake haifahamiki vizuri ni wapi, ingawaje baadhi ya tafiti zinasema kuwa asili yake ni Amerika ya kaskazini.

1. Huimarisha moyo na mifupa

Mbegu za maboga huwa na kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu sambamba na kuongeza ufanisi wa utumbo mpana . Magnesium inaonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshtuko wa moyo na kiharusi.


2. Kinga ya mwili

Mbegu za maboga zina kiwango cha madini aina ya zink, ambayo pia yana faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na na uimarishaji wa kinga mwilini , ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Hali kadhalika zinki huimarisha nguvu za kiume.


3. Saratani ya kibofu

Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinki, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.


4. Ugonjwa wa ini

Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo mbegu hizi zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.


5. Usingizi

Kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kwamba mbegu za maboga zina kirutubisho kinachohamasisha uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi

6. Uvimbe

Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na kuvimba miguu, vidole na hata majipu.


7. Mambo ya kuzingatia

Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizo safi na ambazo hazijakaa muda mrefu, lakini pia tumia mbegu hizo kwa usalama zaidi ikiwa ni sambamba na kuziosha na maji safi na salama kisha zianike na inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini ukila pia baada ya kukaanga bado utapata faida zake. Isipokuwa hakikisha haziungui wakati unapozikaanga unaweza kutumia dakika 10 tu katika zoezi hilo la kuzikaanga.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad