Marekani imesikitishwa na ukamatwaji wa ‘mashoga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Marekani imesikitishwa na ukamatwaji wa ‘mashoga
Taarifa kutoka katika tovuti ya Ubalozi wa Marekani leo November 13, 2018 imeandikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo inasema “Serikali ya Marekani imesikitishwa sana na matukio ya mashambulizi yanayoshamiri na hatua za kisheria zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania, ambazo zinakiuka uhuru wa raia na haki za binadamu, na zinazojenga mazingira ya vurugu, vitisho na ubaguzi.”

“Tunahuzunishwa na hatua za ukamataji watu unaoendelea na unyanyasaji wa makundi maalum, wakiwemo mashoga, na wengine wanaotaka kutumia haki zao za uhuru wa kujieleza, kushiriki na kukusanyika. Vyombo vya kisheria vinatumika kudhibiti uhuru wa raia kwa wote.”

Bado ninainukuu taarifa hiyo ya Marekani “Kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania kunakwamisha maendeleo, ustawi wa uchumi,  amani na usalama. Tunatoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuchukua hatua za makusudi kulinda haki za asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya, wanaharakati wa kisiasa na watu wote kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu, na makubaliano ambayo  nchi imeridhia kikanda na kimataifa.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makundi maalum? eeeh!! eti kukamatwa kwao kunakwamisha maendeleo, kweli?

    ReplyDelete

Top Post Ad