Rais Magufuli Kuwa Mgeni Rasim Sherehe za Baraza la Maulid -Tanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Kuwa Mgeni RasimSherehe za Baraza la Maulid -Tanga
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Maulid litakalofanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga.



Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amesema leo, Jumanne Novemba 13, 2018,  kuwa baraza hilo limeandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) ambapo Maulid hayo ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yatafanyika Novemba 19.



Aidha, amewataka wananchi wa Tanga na mikoa jirani kuhakikisha wanafika kwenye maulidi hayo yanayofanyika mara moja kwa mwaka, huku akisema kuchaguliwa mkoa huo ni bahati hivyo wajitokeze kwa wingi.



Kiongozi huyo wa kiroho, amekemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini akisema hatua hiyo ndiyo chanzo cha vijana wengi kupiga picha za utupu bila aibu na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii na kwamba vitendo hivyo vinavunja hadhi ya nchi na kuomba waliofanya hivyo wakadhibitika sheria kali zichukuliwe dhidi yao ili angalau kukomesha hali hiyo inayotia doa taifa kwa ujumla.



”Hii inasababishwa na malezi mabaya nyumbani kwani mtu mwenye akili timamu hawezi kuvunja heshima yake kwa kuweka picha chafu za kwenye mitandao ya kijamii huo ni uvunjifu wa maadili kwa kiasi kikubwa,” amesema



Alisema mengi yanayohusu kukemea tabia hiyo yataongelewa na watu maalum kwenye maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa baraza hilo hapa nchini ambalo lilianzishwa mwaka 1968 mpaka sasa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad