TCU Yafyekelea Mbali Vyuo Vikuu 12

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TCU Yafyekelea Mbali Vyuo Vikuu 12
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imeendelea kutoa adhabu ya kuvifutia udahili vyuo mbalimbali nchini ambapo mpaka sasa tume hiyo imeshavifutia udahili vyuo 12 nchini na kuvitaka vyuo husika kufanyia marekebisho baadhi ya maelekezo waliyopewa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa TCU Profesa  Charles Kihampa amesema katika kipindi cha mwaka 2018/2019 tume hiyo imefungia vyuo vikuu 10 na kutangaza vyuo vipya 2 walivyofungia.

"Mpaka kufikia sasa vyuo vikuu 12 tumevifutia udahili na haviruhusiwi kudahili wanafunzi wapya mpaka pale watakapomilisha baadhi ya maelekezo ambayo tume imewapa na katika mda waliopewa na kuhakikisha kuendelea kuvifanyia ukaguzi wa mara kwa mara."

Katika taarifa yake Katibu Mtendaji wa TCU Charles Kihampa amesema pia imefuta udahili baadhi ya masomo katika vyuo vya IMTU, Chuo cha
Mtakatifu James, Chuo cha Stefano Moshi pamoja na Chuo cha Sebastian Koloa.

"Tume pia imeendelea kusitisha udahili wa vyuo vikuu viwili ni chuo kikuu kishiriki cha Afya Ifakara Morogoro, na Chuo cha Mtakatifu Mihayo Morogoro mpaka tume itakapojiridhisha," ameongeza Prof Kihampa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad