11/30/2018

Wema Sepetu Afunguka Baada Ya Skendo Yake Nzito

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuelezeawmaisha yake yanavyoenda tangu akumbwe na ile fedheha ya mwaka Baada ya picha na video zake chafu kuvuja mtandaoni.

Wiki chache zilizopita Wema aliwadhangaza watu wengi Baada ya kuamua kuwanika video na picha zake kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha akiwa anakumbatiana kubusiana na aliyekuwa Mpenzi Wake kwa kipindi hiko PCK.

Baada ya sakata hilo Wema amefunguka na kusema kuwa maisha yake ya sasa  anapenda yawe ya siri zaidi na kama ana shida ya kuzungumza vitu ambavyo vinamsibu ni vyema amtafute mtu sahihi ambaye anamuamini kwa asilimia zote.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa, kwa sasa amekuwa makini kwa kila kitu anachofanya ili kumuweka salama tofauti na zamani ambapo mambo yake mengi yalikuwa yakivuja hovyo.

Kwa kweli sasa hivi niko makini sana na kila jambo hivyo nimepitia kipindi kigumu sana mpaka sasa hivi nimeamua kujituliza kufanya vitu vyangu kiakili“.

Baada ya kusambaza picha hizo Wema alifunguliwa kesi mahakamani ambayo inaendelea kusikilizwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger