11/13/2018

Yanga Yatangaza Maamuzi ya Dharura

Yanga Yatangaza Maamuzi ya Dharura
Uongozi wa Klabu ya Yanga Afrika leo Novemba 12, 2018, umefikia maamuzi ya kuitisha mkutano Mkuu wa dharura wa klabu hiyo utakaofanyika tarehe 24 Novemba.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo usiku huu, ajenda bado haijawekwa wazi ila inadaiwa kuwa ni kuweka azimio la pamoja la uchaguzi mkuu wa klabu hiyo usiguse nafasi ya Mwenyekiti.

Pamoja na kueleza tarehe husika ya mkutano huo mkuu wa dharura lakini haijaelezwa ni ukumbi gani utafanyika hivyo kuendelea kuwepo kwa sintofahamu hususani wakati huu ambapo kuna mvuto kuhusu uchaguzi.

Yanga kwa sasa wapo katika mvutano na kamati ya uchaguzi ya shirikisho la mpira Tanzania (TFF) ambao inawataka Yanga kufanya uchaguzi mkuu kuwachagua viongozi wa nafasi mbalimbali lakini wao hawakubaliani na hilo kwa madai kuwa mwenyekiti wao Yusuf Manji bado yupo katika nafasi hiyo.

Jana Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa Yanga George Mkuchika alitangaza kuwa amepokea barua ya Yusuf Manji kutaka kuendelea na nafasi yake hiyo kama kawaida.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF Malangwe Mchungahela amethibitisha kuwa mchakato wa uchaguzi mkuu Yanga utafanyika Januari 13 2019 kama ulivyopangwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger