11/09/2018

Zahera: Siwesi Kuiacha Yanga Hata kwa Fedha Yoyote Ile

Zahera: Siwesi Kuiacha Yanga Hata kwa Fedha Yoyote Ile
KOCHA mkuu wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amefunguka kuwa hata apate ofa ya dola 40,000(Sh90milioni) hawezi kuiacha Yanga sababu maisha sio fedha tu.

Kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa na DRC Congo alijiunga na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita akichukua mikoba ya Mzambia, George Lwandamina.

Mkongo huyo tangu aanze kuinoa Yanga msimu huu katika Ligi Kuu Bara hajapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya sare mbili dhidi ya Simba na Ndanda FC.“Siwezi kuondoka wala kuiacha Yanga sababu ya pesa hata wanilipe kiasi cha Dola 40,000 sababu maisha sio pesa tu bali na kuvumilia na kupambana usiku na mchana kuweza kuisaidia timu.

“Wachezaji wanatakiwa wavumilie na wajitolee kwa kila mechi kwa kupambana kuhakikisha timu inafanya vyema napenda kuona wachezaji wangu wanashinda nyakati zote au naweza kusema Yanga ikifa na mimi nakufa nayo,” alisema Zahera.Kuhusu straika Heritier Makambo alisema; “Makambo kafunga goli nne bado anasemwa kuwa hafungi na mambo mengine mengi ila mnatakiwa kujua hata Ronaldo alivyotoka Madrid kwenda Juventus zilipita mechi tano bila goli ni jambo la kawaida.

“Huyu Makambo katoka kwenye ligi kubwa ambayo ina timu kubwa kama TP Mazembe, Vita Club na nyingine na alikuwa anafanya vyema na kufunga mabao mengi tu hivyo hapa hawezi shindwa.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger