Ahukumiwa Kifo na Baada ya Kukutwa Akifanya Biashara ya Dawa za Kulevya Malaysia

Ahukumiwa Kifo na Baada ya Kukutwa Akifanya Biashara ya Dawa za Kulevya Malaysia
Manaume Sidrey Shalod Dike (46), raia wa Nigeria amehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama nchini Malaysia, baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha na kuingiza nchini humo madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine yenye uzito wa gramu 727.1Kwa mujibu wa Gazeti la New Straits Times (NST) la nchini Malaysia, Dike alikamatwa Mei 3, 2017 na baadaye kupandishwa kizimbani ambapo baada ya kesi yake kunguruma kwa zaidi ya mwaka mmoja, amekutwa na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifo.“Baada ya kupitia hoja zote za upande wa mashtaka na upande wa utetezi, mahakama imebaini pasipo na shaka kwamba mtuhumiwa alifanya kitendo hicho na kumkuta na hatia hivyo namhukumu adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria,” Jaji Datuk Azman Abdullah aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alisema Ijumaa ya Novemba 30, 2018 wakati akisoma hukumu.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Ahukumiwa Kifo na Baada ya Kukutwa Akifanya Biashara ya Dawa za Kulevya Malaysia Ahukumiwa Kifo na Baada ya Kukutwa Akifanya Biashara ya Dawa za Kulevya Malaysia Reviewed by Udaku Special on December 03, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.