12/06/2018

Alikiba Awapa Fursa Mashabiki Zake Kumchagulia Ngoma za Kuimba

AlikibaAwapa Fulsa  Mashabiki Kumchagulia Ngoma za KuimbaMkali wa muziki wa Bongofleva Alikiba amesisitiza uwepo wa tamasha lake la kufunga mwaka ambalo atashirikiana na msanii kutoka Afrika Kusini Yvonne Chakachaka huku akiwaomba amshabiki kumpangia ngoma za kuimba siku hiyo.

Alikiba ambaye ameshaweka wazi kuwa atafunga mwaka kwa kuwa na tamasha la 'Funga Mwaka na KingKiba', leo amethibitisha kuwa amekutana na Yvonne Chakachaka kwaajili ya maandalizi ya awali ya tamasha hilo.

''Show ya kwanza nipo hapa na Mama Yvonne Chakachaka, tunafanya 'set list'. Ungependa tuimbe nyimbo gani siku hiyo ya tarehe 22 December'', ? amewauliza mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Novemba 29, 2018 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa, msani huyo aliitumia kutangaza ujio wa matamasha mawili ya kufunga mwaka ambayo yote yatafanyika jijini Dar es salaam Desemba 22 na 29.
TAZAMA ALICHOFANYA ROSA REE BAADA YA KUFUNGULIWA NA BASATA

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger