12/03/2018

Daimond Kiboko yao Atambulisha Ndege ya Wasafi Festival

Daimond Kiboko Atambulisha Ndege ya Wasafi Festival

Hatimaye Bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz ‘ leo kupitia akaunti yake ya instagram ametambulisha ndege itakayotumika kuwabeba Crew ya wasanii wa Wasafi Festival watakayotumia kwenda Mombasa nchini Kenya Desemba 26, mwaka huu.Ndege hiyo inadaiwa kuandaliwa na waandaaji wa shoo hiyo ambapo watatumia wasanii wa WCB kuwachukua jijini Dar na kuwapeleka Mombasa maalum kwa ajili ya shoo huku wengine wakidai amenunua Diamond japo mwenyewe bado hajaweka wazi kama ni ya kununua ama ya kukodi.


Katika picha aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, ndege hiyo inaonekana ikiwa imezungukwa na mafundi wakiendelea kuibandika stika za Wasafi Festival kwa nje.Hiki ndicho alichokisema Diamond kupitia page yako hiyo “#MchezoUsiuchezeeWewe #kaaaaaaaaaaaaaaaabisa MOMBASA!!! MOMBASA!!!! Now you know #WasafiFestival2018 it’s More than SERIOUS….. See you Dec 26th For Wasafi Festival in MOMBASA!!!!! @nrgradioke 🔥🔥🔥🔥🔥 MOROGORO niko kwa Njia Now, Tukutane JAMUHURI STADIUM!!!

Baada ya kufanya vizuri Mtwara na Iringa, Tamasha la Wasafi Festival linatarajiwa kuendelea leo katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger