12/06/2018

Huu Hapa Ujumbe wa Daimond kwa Mwanaye Nillan Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Msanii wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz ameandika ujumbe mzito kwa Mtoto Wake aliyezaa na Zari The Bosslady Prince Nillan ikiwa ni siku yake ya kusheherekea birthday yake.

Siku ya Leo Nillan anafikisha umri wa miaka mieili pamoja na kuwepo maneno Mengi kwenye mitandao ya kijamii tangu anazaliwa kuwa sio Mtoto wa Diamond lakini Diamond amesema siku zote ni Mtoto Wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amemuandikia ujumbe mzito mtoto wake huyo na kusema:


Miaka miwili iliyopita Mungu alinibariki na Mtoto wangu wa kwanza wa kiume naye nilimuita jina la Nillan linalomaanisha Mwezi/ Asili/ Umaarufu/ Handsome na ni handsome kweli anayeng’aa zaidi ya nyota Happy Birthday Nillan Baba anakupenda”.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger