12/16/2018

Jack Wolper 'Siwezi Kurudia Matapishi ya Mkongo'


MKALI wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa hawezi kurudisha mapenzi kwa mpenzi wake wa zamani ambaye ni Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Putin Kabalu akidai kamwe hawezi kurudia matapishi yake na hana desturi hiyo. 

Akizungumza na Ijumaa, Wolper alisema kuna watu wamekuwa wakivumisha kwamba amerudisha mapenzi kwa Mkongo huyo kwa sababu tu wanapostiana picha kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, lakini hiyo siyo sababu ya kurudisha penzi lao la nyuma bali wanafanya hivyo kimazoea tu.

“Watu wanaonijua vizuri wanafahamu, siwezi kurudia matapishi yangu hata siku moja. Huyo Putin tumekuwa kama washikaji tuliozoeana, lakini hakuna mapenzi tena na hatuwezi kuwa wapenzi tena,” alisema.

 Wolper na Putin walikuwa wapenzi kwa takriban mwaka mmoja ambapo walifikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba, lakini waliachana baada ya mwanaume huyo kugundulika kuwa ana mwanamke mwingine nchini kwao.

Stori: Imelda Mtema


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger