12/16/2018

Kada wa CCM Ajitosa Kuwania Urais 2020


Kada wa CCM, ambaye mwaka 2015 alijitosa kuwania kupitishwa na chama hicho kuwania urais, Dk Muzzammil Kalokola ana mpango wa kuingia tena kwenye mbio hizo mwaka 2020, na hivyo kuwa mpinzani wa kwanza wa Rais John Magufuli.

 

Kada huyo Mkongwe wa CCM, amedai moja ya sababu kubwa ambayo imemfanya aweke wazi hilo ni Mwenyekiti wao wa chama Rais John Magufuli amekuwa akikiuka baadhi ya taratibu za chama hicho ikiwemo kuteua wapinzani katika nyadhifa mbalimbali.


“CCM tulijiwekea utaratibu wa kumuachia Rais kuwa mgombea pekee pale anapomaliza miaka mitano ili akamilishe mitano mingine ili kipindi chake cha miaka 10 kikamilike, lakini Rais Magufuli amekiuka misingi kwa hivyo hakuna sababu ya kumwachia, nitaomba ridhaa nipitishwe.” amesema Dk Kalokola.


“Haiwezekani mtu ambaye wakati wa kampeni za kuwania Urais mwaka 2015 alikuwa akimtukana na kutumia njia zote kuhakikisha Magufuli anakosa urais, leo ametangaza kuingia CCM, kesho jina lake linapitishwa kugombea ubunge, kesho kutwa anakuwa waziri,” alisema Dk Kalokola.


Licha ya Kada huyo kuonesha nia ya kuwania nafasi ya Rais Magufuli, mwingine ambaye alikuwa ametajwa ni aliyekuwa Mbunge wa Mtama, Bernard Membe lakini taratibu za chama hicho zinakataza mtu kutangaza kuwania nafasi ambayo tayari inaongozwa na kiongozi wa chama hicho.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger