Kamati ya Masaa 72 Yawashushia Nyundo Wachezaji Hawa Ligi Kuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kamati ya Masaa 72 Yawashushia Nyundo Wachezaji Hawa Ligi Kuu
Kamati ya saa 72 imewafungia wachezaji  wawili  huku wengine wakipelekwa katika kamati ya nidhamu na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)

 Wachezaji ambao wamefungiwa ni pamoja na Hassan Dilunga wa Simba na Ibrahim Job wa Lipuli  huku mchezaji wa Yanga Andrew Vicent ‘Dante’ na wengine ambao  majina yao hajabainishwa  wamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu.

 Dilunga na Job wamefungiwa kutokana na wachezaji hao kuchelewa kutoka uwanjani wakati timu zikienda kwenye mapumziko kitendo ambacho sio sahihi wakati wenzao wakiwa vyumbani.

Kaimu Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayela amesema kuwa wachezaji wamesimamishwa kwa mechi tatu na wengine wamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu.

“Dilunga na Job wamefungiwa mechi tatu na tayari wameanza kutumikia adhabu zao sababu klabu zilishaarifiwa na watalipa faini ya kiasi cha shilingi laki tano kila mmoja.

 “Wachezaji kama Vicent Andrew wa Yanga pamoja na viongozi wengine wamepelekwa  katika kamati ya nidhamu na hadhi za wachezaji kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu," alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad