Kesi ya Mbowe na Ester Matiko Yapigwa Kalenda Warudishwa Rumande

Kesi ya Mbowe na Ester Matiko Yapigwa Kalenda Warudishwa Rumande
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi inayowakabili viongozi wa CHADEMA, hadi Disemba 21 kwaajili ya kutajwa wakati ikisubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka kupinga usikilizwaji wa rufaa ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge wa Ester Matiko.


Aidha Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri ameridhia taarifa ya kutofika mahakama kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ambao wako nchini Burundi wakishiriki michuano ya mabunge ya Afrika Mashariki.

Hakimu mkazi huyo na upande wa mashtaka wamesema hawana pingamizi juu ya uwepo wa taarifa za uzuru huo kutokana na kupokea nakala za barua za ruhusa kutokana Bungeni.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Kesi ya Mbowe na Ester Matiko Yapigwa Kalenda Warudishwa Rumande Kesi ya Mbowe na Ester Matiko Yapigwa Kalenda Warudishwa Rumande Reviewed by Udaku Special on December 06, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.