12/16/2018

Kimenuka...Msanii wa The Mafik Akamatwa kwa wizi 
Wasanii wanaounda kundi la The Mafik, Hamadai (kushoto) Mbalamwezi (kati kati) na Rhino (kulia)
Msanii wa kundi la The Mafik anayejulikana kwa jina la Mbalamwezi, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi.


Tukio hilo limetokea hapo jana baada ya msanii huyo kumuibia dereva wa gari ya moja ya kampuni zinazotoa huduma za usafiri binafsi jijini Dar es salaam (Taxify), aliyejulikana kwa jina la Calvin.

Akisimulia tukio hilo Calvin amesema Mbalamwezi aliitisha usafiri akitumia simu ya mwenzake, lakini alipokuwa njiani alionekana kuwapigia simu watu kuomba hela kwani hakuwa na pesa ya kumlipa dereva, na ndipo alipochukua uamuzi wa kumuibia dereva baada ya kumfanya apoteze fahamu.

Meneja wa kundi la The Mafik aliyejitambulisha kwa jina la Kapasta amesema ni kweli kuna hilo tukio, lakini ndio yuko njiani akielekea kituo cha Polisi Oysterbay ambako msanii huyo amewekwa rumande ili ajue kinachoendelea.

East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro, lakini alijibu hawezi kuzungumza kwa wakati huo kwani alikuwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu.

Msikilize hapa dereva akisimulia tukio hilo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger