Lukaku Atoboa Siri Aliyoambiwa na Morinyo Kabla ya Mchezo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lukaku Atoboa Siri Aliyoambiwa na Morinyo Kabla ya Mchezo
Mchezaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku amefunguka na kuweka wazi kile alichoambiwa na kocha wake Mreno Jose Mourinho kabla ya mchezo wao dhidi ya Fulham.



Katika mchezo huo ambao ulifanyika katika dimba linalomilikiwa na Manchester United, Old Trafford United walifanikiwa kupata ushindi mkubwa kwa mara ya kwanza msimu huu kwa kupata jumla ya goli 4-1, huku Lukaku akihusika katika goli la tatu akifunga dakika ya 42, huku goli la kwanza likifungwa na Ashley Young mnamo dakika ya 13 ,goli la pili Mhispania Juan Mata dakika ya 28 na goli la nne likifungwa na Muingereza Marcos Rashford dakika ya 82 nagoli la Fulham la kufutia machozi likipatikana dakika ya 67 kwa mkwaju wa penati huku mnamo dakika ya 68 Mcameroon André-Frank Zambo Anguissa akilamba kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Rashford ambapo alionyeshwa kadi ya pili ya njano.



Katika mahojiano ya Lukaku na Skysport, mchezaji huyo amefunguka haya ambayo anadai ndio yalimsaidia katika mchezo huo, na maneno haya akisema aliambiwa na kocha wake Mourinho.



“Nadhani ninahitaji tu kuendelea kufanya kazi kwa bidii. Mimi na meneja tulikuwa na majadiliano mazuri katika siku chache zilizopita, ambapo kwa kweli aliniambia nini alitaka kutoka kwangu, Najua kutoka upande wangu ni lazima kufanya vizuri zaidi, na ninaendelea kuangalia mbele na kuboresha, kujaribu kuongeza katika mchezo wangu na kusaidia timu kushinda.”



Alipoulizwa kile ambacho kilikuwa kinapelekea kutokufanya vizuri katika baadhi ya michezo akiwa kama, mshambuliaji akasema: “Sio kwamba hakufanya vibaya sana. Nilikuwa nacheza bila shinikizo la kutosha, nadhani dhidi ya Fulham nilicheza kwa nguvu kama kila mtu alivyofanya, Kwa mimi nilifurahi kucheza kwenye kiwango kizuri, yote kuhusu kuboresha na kuendelea kwa msingi thabiti.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad