12/06/2018

Mama Diamond Avunja Ukimya Kuhusu Mpenzi Mpya Wa Diamond


Mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz   Bi. Sandrah amefunguka na kumuongelea Mpenzi mpya wa Diamond anayejulikana kama Tanasha Donna Oketh mwenye ajili ya Kenya.

Wiki iliyopita Diamond alishangaza watu wengi Baada ya kutangaza ndoa na Mpenzi Wake Mpya Tanasha itakayofungwa 14 February 2019 ilihali alikuwa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na Kimnana.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko linaripoti kuwa kumekuwa na taarifa za chini chini kuwa Mama Diamond hamtaki kabisa Tanasha kwa sababu alikuwa anamkubali Kim Nana ambaye alikuwa tayari kubadilisha dini na alikuwa kashaanza kufundishwa Quran tayari kwa ajili ya ndoa na Diamond.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi, Mama Diamond alianza kwa kukanusha habari kuwa alimkataa mrembo huyo na kwamba alikuwa anamtaka Kim Nana. Mama Diamond alisema anamkubali Tanasha kwa moyo mmoja wala hana kipingamizi naye na ikitokea mwanaye kweli anataka kumuoa, basi yupo radhi wala hana shida.

Sasa nimkatae amenikosea nini mtoto wa watu? Nani amesema nimemkataa mkwe wangu? Kama  mwanangu amemuona anamfaa basi nipo radhi amuoe maana umri Wake unaenda na umri wa kumuoa ndio huu”.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger