AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Kauli hiyo ya Mbowe imetolewa Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara na mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya kusikilizwa rufaa ya kupata au kutopata dhamana kwa viongozi hao wawili.
"Mwenyekiti amesisitiza sana, kutomlilia yeye bali walilie taifa letu kutafuta mabadiliko, kudai tume huru ya uchaguzi, kwa sababu kesi hii msingi wake ni uchaguzi uliosababisha kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina kwa hiyo naomba wajitokeze kwa waingi kesho," amesema Mnyika.
Wakati huohuo Mnyika amebainisha kuwa chama hicho kupitia mawakili wake kimewasilisha maombi ya kuiomba mahakama kutoa kipaumbele kwa kesi dhdi ya viongozi wake kabla ya mahakama hiyo haijaenda likizo.
Mbowe na Matiko wako mahabusu baada ya kufutiwa dhamana kwenye kesi yao ya msingi inayowakabili juu ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwilini ambapo walifutiwa dhamana hiyo kwa madai ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK