Mhandisi atiwa mbaroni kwa kuomba rushwa ya ngono

Mhandisi atiwa mbaroni kwa kuomba rushwa ya ngono
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) jijini Dar inamshikilia Mhandisi wa Kampuni ya Mask and Sons, Leonard Mkaka kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono

TAKUKURU ilimuwekea mtego katika nyumba ya kulala Wageni ya Nara Beach Lodge iliyoko Kigamboni na kufanikiwa kumkamata

Kampuni anayofanyia kazi imepewa zabuni ya kutengeneza barabara katika Halmashauri ya Temeke maeneo ya Toangoma mtaa wa Masaki jijini humo

Anaelezwa kuvunja kifungu cha 25 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2017 na atafikishwa Mahakamani kufunguliwa mashtaka

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Mhandisi atiwa mbaroni kwa kuomba rushwa ya ngono Mhandisi atiwa mbaroni kwa kuomba rushwa ya ngono Reviewed by Udaku Special on December 06, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.