12/15/2018

Mlinzi wa Uhuru Aonekana na Mkono Bandia Kwenye Mpango wa Siri wa Usalama


-Mlinzi wa siri wa Rais Uhuru Kenyatta alionekana akiwa na mkono wa kushoto uliokuwa na rangi tofauti na mkono wake wa kulia

-Mkono huo haukuwa ukisonga na wachanganuzi walidai kuwa ulikuwa mkono wa kutengenezwa na kuwekwa mwilini

-Watu wengine walidai kuwa mkono huo ulikuwa bandia na ulificha silaha hatari kwenye koti lake

-Walinzi wa rais wa Marekani Donald Trump pia walionekana na mkono kama huo wakati wa kuapishwa kwake Ijumaa, Januari 20, 2017

Sherehe ya 55 ya Jamhuri ilishuhudia mbwembwe nyingi hasa ile ya Rais Uhuru Kenyatta kuvalia vazi nyekundu rasmi la kijeshi la hafla na kumpigia saluti mkewe Margaret Kenyatta.

Walinzi wengi waliokuwa kwenye hafla hiyo walijizatiti kuhakikisha kuwa usalama wa rais na umati kwenye uwanja huo umedumishwa.

Hata hivyo, raia waligundua kuwa mmoja wa walinzi wa rais alikuwa na mkono bandia ambao rangi yake ulikuwa tofauti na ule wa mkono wake mwingine.

Wengi walisema kuwa mlinzi husika aliyekuwa akitembea karibu na rais katika uwanja wa Nyayo alikuwa na mkono wa kushoto wa kutengenezwa, kisa na maana haukuonekana ukisonga.

Tukio hilo lilikuwa sawia na lile la hafla ya kuapishwa kwa rais wa Marekani Ijumaa, Januari 20, 2017 ambapo mlinzi mmoja wa rais huyo alionekana kuwa na mkono bandia sawia na ule wa mlinzi wa Uhuru.

TUKO.co.ke ilibaini kuwa huduma ya walinzi wa rais ilitumia bunduki za hali ya juu ikiwemo ile ya mfumo wa ‘lanyard’ kutoa ulinzi kwa watu mashuhuri wakati wa hatari.

Kwenye mpango huo, suti hutengenezwa kwa mkono bandia huku mkono halisi wa mlinzi ulio ndani ya mkono huo bandia ukiwa umeshika bunduki tayari kukabiliana na hali r huo wa ulinzi pia umetumika na majeshi ya Israeli.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger