Mwalimu Hatarini Kwenda Jela Kisa Kumnyoa Nywele Mwanafunzi Kwa Lazima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwalimu Hatarini Kwenda Jela Kisa Kumnyoa Nywele Mwanafunzi Kwa Lazima
Mwalimu mmoja nchini Marekani anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu, baada ya picha ya video kusambaa mitandaoni akimkata kwa lazima nywele mwanafunzi mmoja darasani, huku akiimba wimbo wa taifa wa Marekani.

Margaret Gieszinger, 52, amefukuzwa kazi kwa kitendo hicho alichokifanya katika Shule ya Sekondari ya Chuo Kikuu cha huko Visalia, California.

Waendesha mashtaka wamesema kuwa amekanusha makosa sita dhidi yake, likiwemo kosa la ukatili dhidi ya mtoto na . Anakabiliwa na hukumu ya miaka mitatu u nusu jela.

Bi Gieszinger, aliachiliwa kwa dhamana ya dola 100,000 Ijumaa jioni.

Katika video hiyo ya rununu iliyowekwa mtandaoni na Reddit, anayefunza somo la Sayansi, mshtakiwa anaonekana akimuita mwanafunzi wa kiume kuketi mbele ya darasa, kisha akanza kumkatakata nywele huku akiimba wimbo usio rasmi wa nyota wa muziki Spangled Banner.

Wakili wa mwanafunzi huyo, ameliambia shirika la habari la CNN kuwa, mteja wake

"alishtuka sana" kabla ya kufaulu kujinasua mikononi mwa mwalimu huyo.

Bi Gieszinger kisha anaonekana kwenye video, akishika mkasi mkononi juu ya kichwa chake na kusema "next!" yaani "mwingine!" na kutishi pia kumkata nywele mwanafunzi mmoja wa kike.

"Tunachukulia kwa tahadhari kubwa mno usalama wa wanafunzi madarasani," hiyo ni kwa mjibu wa tarifa kutoka kwa afisi kuu ya Elimu ya kaunti ya Tulare.

"Tunachunguza taarifa zote tunazozipokea na tutachukua hatua kali mno na zinazohitajika dhidi ya wafanyikazi wetu walio na utovu wa nidhamu." Taarifa hiyo imeongeza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad