12/06/2018

“Nampenda Sana Wifi Yangu Tanasha”-Esma Platnumz

“Nampenda Sana Wifi Yangu Tanasha”-Esma Platnumz
Dada wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kusema hana neno na wifi yake mpya Tanasha Donna Oketh.

Wiki iliyopita Diamond alimtambulisha Mpenzi Wake Mpya na mara moja kutangaza kuwa ana mpango wa Kumuoa itakapofika mwakani tarehe 14 February.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi, Esma ambaye alikuwa beneti na Tanasha alifunguka kuwa kwa upande wake alimpokea wifi yake mpya kwa mikono miwili.Esma ambaye amepachikwa jina la Yuda mitandaoni kutokana na kuwageuka warembo ambao huwa wanakuwa na Diamond kisha kupigwa kibuti alisema:

Wala sina shida, nimemkubali wifi yangu na kwa sababu Nasibu (Diamond) mwenyewe ndiye amesema anamuoa na ameridhiana naye, mimi ni nani nikatae?

Kikubwa ninawaombea heri tu asiwe kama wengine ili na mimi nipate wifi wa halali, niache uyuda”.

Mashabiki wameituhumu familia ya Diamond kwa unafiki kwani Wiki mbili tu zilizopita walionekana na Kim Nana na hata Mama Diamond alisema mume Wake anamfundisha dini ili aweze kubadilisha dini na kuolewa na Diamond.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger