Rais wa TLS ataja vitu vinavyomharibu Mwanaume

Rais wa TLS ataja vitu vinavyomharibu Mwanaume
Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Fatma Karume ametoa maoni yake juu ya kitu kinachowaharibu wanaume huwa ni pesa na madaraka na si kingine, wengi wao hugeuka na kuanza kufanya vitendo vya kikatili.

Ameandika hivi katika Twitter yake “Vitu viwili vinamharibu mwanaume dhaifu, pesa na madaraka. Akishayapata hayo mawili anapofuka macho na anakua kiziwi ispokua pale anaposifiwa tu”.

Pia akaandika tena “Mwanamke dhaifu anakua hatari pale anapokua anauchu wa pesa au madaraka. Anaweza kufanya chochote ili apate haya. See Gender Neutral”

Fatma anaandika haya wakati jamii ikiwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) umesema mwanamke mmoja katika kila wanawake watatu  amewahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia, kimwili, kingono au kisaikolojia.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Rais wa TLS ataja vitu vinavyomharibu Mwanaume Rais wa TLS ataja vitu vinavyomharibu Mwanaume Reviewed by Udaku Special on December 06, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.