12/05/2018

Rosa Muhando Alazwa ICU Kenya


DUA zinahitajika kutokana na madai kwamba, nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.  Chanzo makini kutoka nchi hiyo jirani kilieleza kuwa, hali ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kibao kama Nibebe, Nipe Uvumilivu na nyingine nyingi kwa sasa yupo hospitali akisumbuliwa na maradhi ikiwemo mikono inayotajwa kuwa imeharibika. Kilieleza kuwa, baada ya Rose kushindikana kupata nafuu kanisani alikokuwa anafanyiwa maombi, mwenyeji wake ambaye naye ni mwimbaji wa injili pamoja na wenzake walimpeleka hospitali (haikutajwa) kwa tiba zaidi.

“Kwa sasa yupo ICU huku Kenya ambapo suala la afya yake liko mikononi mwa baadhi ya waimbaji Injili wa huku ambao wamekuwa wakifanya siri ili watu wasijue kama Rose kalazwa. “Ukweli haujulikani kalazwa hospitali gani, lakini kuna madai kuwa ameathiriwa sana na madawa ya kulevya hivyo wanahofia wakitaja jina la hospitali kila mtu atajua chanzo cha kuumwa kwake.

“Mimi nimeambiwa kinachomsumbua ni mikono ambayo hata kwenye video iliyosambaa hivi karibuni mitandaoni ilionekana kama imeungua moto, yapo madai kuwa mikono imeanza kuoza na hawezi kufanya kitu chochote,” kilidai chanzo. Inaelezwa kwamba, hapo hospitali ameambiwa atakaa kwa siku 30 kwa ajili ya matibabu na ushauri, hivyo hawezi kurudi Tanzania hadi apate nafuu.

Ili kuujua ukweli wa habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kiongozi wa chama cha waimba Injili cha Tanzania Music Foundation ‘TAMUFO’, Stella Joel ambaye alisema, wamesikia taarifa hizo za kulazwa kwa Rose lakini wao kama chama wanafuatilia zaidi. “Tumesikia Rose amelazwa Kenya hivyo tunafuatilia na tukishapata ripoti kamili tutatoa taarifa zaidi,” alisema Stella.

TUJIKUMBUSHE

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha Rose akiwa amedhoofu mwili huku mikono na uso vikiwa kama vimeungua moto ambapo mchungaji alikuwa akimuombea na Rose kuonekana amepagawa na mapepo. Video hiyo ilizua gumzo hasa kutokana na wadadisi wa mambo kutilia shaka maneno aliyokuwa anatamka wakati akiwa amepagawa na mapepo ambayo yalitajwa kuwa kama yamepangwa kwa lengo maalumu ambalo lilidaiwa kuwa ni kutafuta kiki.

Stori:GLADNESS MALLYA, RISASI MCHANGANYIKO
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger