Simba Kuwafuata Nkana Jumatano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Simba Kuwafuata Nkana Jumatano
KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Jumatano kwa mafungu kuelekea nchini Zambia ili kuwakabili wapinzani wao Nkana FC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.



Simba itakuwa ugenini kucheza na Nkana Jumamosi na marudio yanatarajiwa kuwa Desemba 23 au 24 Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa.



Akizungumza na Championi Jumatatu, Katibu wa Simba, Dr. Arnold Kashembe, alisema kuwa maandalizi ya timu yapo sawa na wanatarajia kuondoka kimafungu kwa kuwa kuna wengine ambao wameshatangulia kuweka mipango sawa huku wengine wakifuata kuungana nao baadaye.



“Mpaka sasa tumeshatambua kuwa aina ya timu tunayokwenda kucheza nayo ni ngumu, hivyo tumedhamiria kupata matokeo mazuri, kwa kuanza safari yetu tunajigawa makundi kufika Zambia kwa kuwa hatuwezi kwenda wote kwa wakati mmoja.



“Taratibu zote zipo sawa na uhakika wa kufanya vizuri ni mkubwa na ndiyo maana kuna watu ambao wametangulia kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya timu yetu, kuhusu kuondoka kwa wachezaji na viongozi utaratibu utakuwa wazi hivyo Watanzania na mashabiki sapoti yenu muhimu,” alisema Kashembe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad