12/01/2018

Tyson Fury Asema Kupigana na Wilder Leo ni Sherehe


Mwanamasumbwi wa Uingereza Tyson Fury amesema pambano lake la leo kuwania mkanda wa dunia wa WBC uzito wa juu dhidi ya Deontay Wilder, ni kama sherehe kwake kutokana na kurejea kutoka kwenye mapumziko.

Fury mwenye miaka 30 anakutana na Wilder leo huko mjini Los Angeles ikiwa ni chini ya miezi sita baada ya kuwa nje miezi 30, ambapo alikuwa anapambana na tatizo la msongo wa mawazo pamoja na kifungo cha miezi 30 kutoka kwa mamlaka ya kupambana na dawa za kuongeza nguvu michezoni ya nchini Uingereza.

''Hii kwangu ni siku muhimu ya furaha, hakuna bondia amewahi kutoka kupumzika akacheza pambano kubwa kama hili hivyo naichukulia kama sherehe na nitapata ushindi lakini kukubwa nalifurahia sana'', amesema Fury.

Fury anaripotiwa kuwa ngumzo nchini Marekani kutokana na kufanikiwa kukata uzito kwa kupunguza kilo 20 ndani ya miezi 12 na jana amefuzu vipimo vya uzito kwaajili ya pambano la leo.

Mabondia hao wawili hawajawahi kupoteza pambano ambapo Fury ameshuka ulingoni mara 27 na kushinda yote huku mara 19 ikiwa ni kwa KO. Wilder yeye ameshuka dimbani mara 40 na kushinda yote na 39 ikiwa ni kwa KO.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger